You need to enable JavaScript to run this app.
Nenda kwenye maudhui
Nenda kwenye orodha kuu
Nenda tovuti zaidi za DW
Vidio zetu
Sauti zetu
Maeneo
Tanzania
Kenya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Afrika
Ulaya
Mada
Haki za binadamu
Mazingira
Afya
Teknolojia
Kategoria
Matukio ya Kisiasa
Masuala ya Jamii
Michezo
Yanayoangaziwa
Mzozo wa Kongo Mashariki
Mzozo wa Israel na Hamas
Bundesliga
Sauti zetu
Vidio zetu
Matangazo
Picha: DW
Vidio zetu
Tazama vidio zetu hapa
Ruka sehemu inayofuata Maudhui yote kwenye mada hii
Maudhui yote kwenye mada hii
Filamu ya Kitanzania "Kaburi wazi" yazua mjadala Köln
Athari za ukoloni bado zinashuhudiwa katika mataifa mengi barani Afrika, lakini katika kipindi cha takriban karne moja ya ukoloni wa Ujerumani nchini Tanganyika ambayo ni Tanzania bara ya sasa, Je, Wajerumani wanatilia maanani kile babu zao walikitenda katika taifa hilo la Afrika mashariki? Tazama mjadala na majibu katika filamu ya "Kaburi wazi".
Wasichana wa sasa katika kuzienzi tamaduni zao
Katika safu yetu ya Msichana Jasiri, mjadala unaopewa nafasi unahusu. "Wasichana katika kuzienzi tamaduni zao."
Mafuriko yaacha homa ya mapafu kwa watoto Kenya
Mvua kubwa zilizoambatana na mafuriko zimeacha athari za kiafya kwa watoto wengi katika maeneo ya mabanda nchini Kenya
Msomi wa uchumi na mbunifu wa mapambo ya ndani ya kitamaduni
Kutoka kuwa mwanauchumi mpaka kutumia stadi za mikono katika kujiajiri hii haikuwa rahisi kwake, lakini ule msemo waelimu ni ufunguo wa maisha kwake anautendea haki anaitumia elimu yake ili kuhakikisha kuwa anapata bidhaa zenye ubora na hata kuzitangaza kwa kutumia majukwaa mbalimbali huku akiwa na matarajio ya kufika katika soko la kimataifa.
Wasichana na wanawake wanavyotumia fursa ya teknolojia
Kuwekeza katika elimu ya teknolojia ya akili ya kubuni (AI) kwa wasichana sio tu kunafungua uwezo wao bali pia huchochea uvumbuzi na utofauti katika tasnia ya teknolojia kwa baadae. Taasisi ya LP digital kutoka Tanzania inafanya jukumu hilo la kutoa mwanga wa sayansi bunifu kwa wasichana.
Kutibu majeraha yaliosababishwa na vita Ukraine
Zaidi ya wanajeshi elfu ishirini waliojeruhiwa walifika katika hospitali ya Mechnikov katika eneo la Dnipro, tangu Urusi ilipoivamilia kikamilifu Ukraine mnamo Februari 2022. Daktari Valentyna Lisnycha katika hospitali hiyo inayotibu wanajeshi waliojeruhiwa vitani pamoja na timu yake wamejitolea kuokoa maisha ya askari.
Kurunzi Live: Maoni ya Wananchi juu ya Muungano
Wakati Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ukikaribia kutimiza miaka 60, Watanzania wamekuwa na maoni tofauti kuhusiana na muungano huo. Je wanahisi kama bado una umuhimu kwao ama la? Tizama video hii kwa mengi zaidi, kisha utupe maoni yako.
Wanawake wenye ulemavu wajiunga na mchezo wa mpira wa mikono
Kutana na wanawake hawa wenye ulemavu waliamua kujiingiza kwenye mchezo wa mpira wa mikono na namna wanavyosakata mchezo huo.
Mwanaharakati wa haki za watoto wa mitaani Tanzania
Kundi la watoto wa mtaani ni kundi ambalo linaendelea kuongezeka kwa kasi huku watoto hawa wakiwa hawana elimu madhubuti kutokana na ukatili wanaokutana nao, lakini juhudi za wanaharakati wa masuala ya kijamii ni zipi katika kuhakikisha kuwa wanalisaidia kundi hili. Jackline Joseph ni mwanaharakati ambaye amejitolea katika kulisaidia watoto katika kuwapatia elimu dhidi ya ukatili.
Chipukizi wa muziki wa kizazi kipya
Precious ni mwanamuziki chipukizi wa kizazi kipya kutoka Tanzania ambaye Uwezo wake wa kutumbuiza katika majukwaa umempa sababu ya kuwa mfano kwa watoto wengine. Anasema baba yake ndiye aliyempa msukumo mkubwa wa kunoa kipaji chake. #msichanajasiri.
Umewahi kuombwa ama kutoa rushwa?
Rushwa ni tatizo la Kidunia lenye madhara makubwa kwa mtu, jamii, hadi ngazi ya taifa. Rushwa imetumiwa kupoka haki stahili kwa watu na pengine kumpa yule asiyeistahili ama mpokea rushwa kujinufaisha tu mwenyewe. Kuna nyakati hata sheria hupindishwa kwa sababu ya rushwa. Umewahi kuombwa ama kutoa rushwa ili kupata huduma yoyote ile?
Unalifahamu vipi tatizo la Usonji?
Ugonjwa wa Usonji au Autism ni tatizo la kibaiolojia ambalo kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani, WHO, huathiri mtoto mmoja kati ya kila watoto 100 duniani. Dalili zake huanza kuonekana mapema sana, kuanzia umri wa miaka mitatu na kuendelea. Ni vigumu kugundua dalili zake. Lakini kwenye video hii unaweza kujifunza mengi.
Utafiti: Kiwango cha Umasikini Ujerumani bado kipo juu
Ripoti mpya ya makundi ya ustawi wa jamii Paritätischer Gesamtverband inaonyesha kuwa kiwango cha umaskini nchini Ujerumani bado kipo juu. Takwimu za hivi karibuni zinaonyesha kuwa asilimia 16.8 ya watu wanaishi katika umasikini, hiyo ikiwa ni takriban watu milioni 14.2. Kwa mujibu wa ripoti hali ya umasikini imewaathiri watoto pamoja na kundi la wastaafu.
Wasichana wanavyosherehekea sikukuu ya Pasaka
Katika sikukuu ya pasaka kumekuwa na changamoto nyingi ambazo huwakuta wasichana pale wanapoenda kujivinjari katika viwanja tofauti tofauti lakini vipi wanaweza kuepukana na hayaWasichana wanavyosherehekea sikukuu ya Pasaka
Programu ya simu DigiCow yaleta mapinduzi kwa wafugaji
Peninah Njeri ambae anazitambua changamoto zinazowakabili wafugaji wa ngo'ombe wa maziwa nchini Kenya, ameunda jukwaa la kidijitali ambalo linatoa habari na rasilimali muhimu katika masuala ya ufugaji. DigiCow, imeleta mapinduzi makubwa kwa wafugaji na sasa takriban wafugaji 60,000 barani Afrika wanategemea jukwaa hilo kwa ufugaji wa kisasa.
Joto kali lina athari gani mwilini ?
Daktari Jalab Ashraf atowa maelezo zaidi jinsi ya kuhakikisha tunabakia imara kiafya katika kipindi hiki cha joto kali.
Kivuli cha Ukoloni wa Ujerumani - Sehemu ya Kumi
Katika sehemu ya 10 ya simulizi tunatizama jinsi migogoro ya mipaka inayoshuhudiwa leo nchini Cameroon, Namibia na Tanzania ilivyo na mizizi yake toka enzi ya ukoloni.
Kivuli cha Ukoloni wa Ujerumani - Sehemu ya Tisa
Katika makala hii tunaangalia jinsi wakoloni wa kijerumani walivyotumia nadharia ya rangi tofauti za binadamu ili kuhalalisha udhalimu wa ukoloni wao.
Kivuli cha Ukoloni wa Ujerumani - Sehemu ya Nane
Kwa karne kadhaa sasa matibabu yaliyogunduliwa na mataifa ya magharibi yameokoa maisha ya mamilioni ya watu duniani. Lakini hali haikuwa hivyo katika siku za mwanzo mwanzo za ukoloni wa nchi za Ulaya barani Afrika.
Kivuli cha Ukoloni wa Ujerumani - Sehemu ya Saba
Mara hii tunamuangazia Quane Martin Dibobe, mwanaharakati wa haki za binadamu aliyepinga unyonyaji wa Ujerumani katika makoloni yake.
Kivuli cha ukoloni wa Ujerumani - Sehemu ya Sita
Kwenye sehemu ya 6 ya mfululizo wa simulizi tunaimulika miongo mitatu ya Utawala wa Ujerumani huko Togoland, koloni lililozingatiwa na viongozi mjini Berlin kuwa la mfano kuliko yote barani Afrika.
Kivuli cha Ukoloni wa Ujerumani - Sehemu ya Tano
Tunaendelea na mfululizo wa makala za kivuli cha ukoloni wa wajerumani barani Afrika ambapo hii leo tunaingia kwenye sehemu ya tano.
Kivuli cha Ukoloni wa Ujerumani- Sehemu ya Nne
Mara hii tunamulika mauaji ya kimbari yaliyofanywa na serikali ya ukoloni wa Wajerumani kati ya mwaka 1904 hadi 1908 dhidi ya makabila ya Herero na Nama huko Nambia, Kusini mwa Afrika.
Kivuli cha Ukoloni wa Ujerumani- Sehemu ya Tatu
Sikiliza sehemu hii ya tatu ya mfululizo wa makala zetu juu ya ukoloni barani Afrika.
Kivuli cha Ukoloni wa Ujerumani - Sehemu ya Pili
Sikiliza sehemu hii ya pili ya mfululizo wa makala zetu juu ya ukoloni barani Afrika.
Kivuli cha ukoloni wa Ujerumani - Sehemu ya Kwanza
Kufikia mwaka 1885, mfanyibiashara wa Ujerumani alifanikiwa kununua pwani nzima ya Kiafrika. Alifanya hivyo kwa kutumia bunduki chache alizokuwa nazo pamoja na mkataba wenye hila. Mkataba huo pamoja na mikataba mingine barani Afrika ilifuangua mwanya kwa utawala wa kikoloni wa Ujerumani.
Hisia za kutojiamini
Umewahi kupata hisia za kutojiamini? Wanasaikolojia wanasema hisia hizo huchangiwa na mambo tofauti ikiwemo malezi na tabia binafsi. #Kurunziafya inatizama hisia hizo, ambazo si ugonjwa lakini hutupata katika maisha yetu ya kila siku.
Wasichana jitokezeni kwenye sayansi na teknolojia
Miriam ameona ombwe la wasichana kujitosa katika masomo ya sayansi, kwa nafasi yake mbali na kuwa katika masuala ya sayansi na teknolojia, lakini pia amekuwa muhamasishaji kwa wasichana wengine kujitokeza katika sekta hiyo.
Msichana mdogo anayefanya harakati za kutunza mazingira
Sheila Juma ni msichana mdogo anaeendesha harakati za mwanmake kulinda mazingira kupitia taulo za kike.
Mpango wa kukopa na kulipia deni la matibabu Nigeria
Kutana na kikundi cha kijamii kutoka katika jimbo la Kano kaskazini mwa Nigeria, ambacho kinasaidia kaya masikini kulipa madeni ya matibabu hasa kwenye maduka ya dawa, lakini hata hivyo mpango hausadii tu watu masikini pia unaziwezesha biashara za dawa kustawi.
Jasiri mwenye ndoto za kuwa mwanamasumbwi bora duniani
Kuingia kwake katika mchezo wa ngumi kuliambatana na changamoto nyingi lakini bado anaonesha ari kubwa katika kuziishi ndoto zake. Anatamani kuwa bondia mkubwa ulimwengu lakini ushirikiano anaoupata kutoka kwa watu wake umekua hafifu. Vipi anaweza kuzimudu changamoto hizi ili kufikia malengo yake?
Ulaji wa chakula usiofaa chanzo cha matatizo ya afya
Profesa Janabi wa Muhimbili Tanzania anasema watu hawajakatazwa kula ispokuwa wale kwa mpangilio ili kutunza afya.
Maoni: Mafanikio ya kijana yanahitaji watu wa aina gani?
Wataalamu wanasema mafanikio ni hatua baada ya changamoto chungumzima, lakini kufikia mafanikio inahitaji mtandao wa watu wataofanikisha safari hiyo.Je, unahitaji watu wa aina gani maishani ili kufikia kilele cha mafanikio? Sikio maoni ya vijana wa Kilimanjaro Tanzania
Turakella: Ubaguzi nchini Algeria ulifungua mlango wa fursa
Akiwa katika safari yake ya elimu nchini Algeria msichana Turakella anakumbana na visa vya ubaguzi, ambavyo badala ya kumdhoofisha viligeuka fursa kwake na kuingia katika ulimwengu wa sanaa adimu. Sikia hadithi hii kupitia msichana jasiri
Leila Abdul Kheir na vita dhidi ya utoaji mimba holela
Jamii huepuka kuyajadili maswala ya wanawake hasa yanayohusiana na ujauzito na utoaji mimba kwani huchukuliwa kuwa aibu.
Umeisherehekea vipi sikukuu ya wapendanao?
Haya tuambie leo umeisherehekea vipi siku hii maalumu kwa ajili ya wapendanao? Huko Uganda kila mmoja ana mtizamo wake kuhusiana na siku hii. Tizama kwanza video hii iliyoandaliwa na Lubega Emmanuel, kisha nawe utuambie mtizamo wako.
Binti Jasiri Magreth: Mwenye changamoto ya kusikia
Msichana Magreth Mathias ana changamoto ya kusikia lakini ameweza kuanzisha kampuni yake na kutoa ajira kwa wenzake. Mtazame katika vidio hii ya "Msichana Jasiri"iliyoandaliwa na Mitchelle Ceasar
Matumizi ya akili ya kubuni katika sekta ya afya Ujerumani
Madaktari katika hospitali ya Saarbrücken, Ujerumani wanatumia teknolojia ya akili ya kubuni katika kufanya upasuaji.
Tofauti ya maisha ya mtandaoni na maisha halisi
Mitandao ya kijamii imechukua sehemu kubwa ya maisha ya watu hasa vijana, ila wengi wanaishi maisha "feki."
Israel epusheni mauaji ya halaiki Gaza
Mahakama ya Umoja wa Mataifa ICJ imeiamuru Israel kuzuwia vitendo vya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina, na kuchukua hatua zaidi kuwasaidia raia, ingawa imesita kuamuru usitishaji mapigano kama ambavyo Afrika Kusini ilikuwa imeiomba.
Mapambano ya kiuchumi kwa wasichana na wanawake
Kumuandaa mwanamke wa baadae ni kumuwekea mazingira bora msichana katika kila sekta ili kufikia malengo ya kujitegemea kiuchumi kwenye azma ya kuupiga kumbo umasikini inapofika 2030, lakini kutimiza hilo ni muhimu kumjumuisha kila mmoja, wasichana nao hawajabaki nyuma katika mbio hizo. Ungana na Mitchelle Ceasar katika video ya Msichana Jasiri.
Hamasa ya wahudumu katika vyumba vya kuhifadhi maiti
Wengi wamekuwa na mawazo tofauti juu ya watu wanaotoa huduma katika vyumba vya kujifadhi maiti katika hospitali na utakubali kwamba kumekuwa na hadithi nyingi kuwahusu na wakati mwingine hata zikitia hofu, lakini hebu tazama video usikie hadithi zao wenyewe wakisimulia juu ya hamasa inayowafanya kuipenda kazi yao adhim.
Msichana Jasiri yamuangazia Naishooki Gideon, mhamasishaji
Ongezeko la ukatili wa kijinsia ulimsukuma kuwa mhamasishaji na muelimishaji wa vijana katika jamii. Mtangazaji wetu chipukizi Mitchelle Ceaser anaangazia juhudi zake Naishooki Gideon kwenye vidio yetu ya Msichana Jasiri
Mipaka ya ajabu iliyochorwa na Wakoloni barani Afrika
Watawala wa mwisho wa kikoloni wa Kijerumani waliondoka zaidi ya karne moja iliyopita. Lakini mipaka ya Kiafrika iliyochorwa mjini Berlin mwishoni mwa karne ya 19 bado haijabadilika hadi leo - na imekuwa na matokeo mabaya sana.
Tiba ya jino ya Root Canal
Ni lini mara ya mwisho uliumwa jino? Yale maumivu kiasi cha kuona giza wakati ni mchana😆😆😆 Je huwa una utaratibu wa kwenda kwa daktari wa meno kabla hujakumbwa na zahma kama hii? Na je, ulitibiwaje? Hebu msikie kijana huyu ambaye siku moja alikwenda bila ya kusukumwa hospitalini baada ya kuumwa jino na usikie alitibiwaje? Itakusaidia. #kurunziafya
Mary Angel: Sanaa na muziki nyenzo za elimu ya afya ya akili
Sanaa ni nyezo ambayo hutumika katika kufikisha ujumbe kwa hadhira katika njia tofauti ikiwemo muziki, uchoraji na hata ufinyanzi na katika matumizi haya hapa ndipo anajitokeza msichana ambaye anaamua kuitumia sanaa ya muziki pamopja na uchoraji katika kuelimisha juu ya afya ya akili je nikwanini aliamua kutumia sanaa katika kuelimisha na elezea hisia binafsi? Jua mengi kupitia Msichana Jasiri.
Wasichana wachukua mwelekeo mpya wa ngoma za asili
Licha ya kutawala kwa muziki na midundo ya kisasa ambayo inawapagawisha watu wengi, lakini bado ladha ya ngoma za asili zimebaki kuwa pendwa miongoni mwa wengi. Wasichana wa kundi la Shine wanajifua kuunga'arisha muziki huo na kuutegemea kama ajira katika maisha yao ya baadae.
Kwa nini Afrika bado inapigania mipaka ya wakoloni?
Mipaka ya Afrika iliyochorwa Berlin mwishoni mwa karne ya 19 bado ipo na imekuwa na madhara mabaya sana.
Ukoloni ulivyochangia ukosefu wa imani kwa dawa za Magharibi
Mateso haya yasiyozungumzwa yanaelezea kwa nini kuna uzito wa kuzikubali chanjo hizo hadi leo.
Uhusiano baina ya ugozi wa zama za ukoloni na unazi
Wasomi walioheshimika walijijengea majina makubwa kwa kuasisi na kuitetea nadharia chafu ya ugozi.
Ukurasa uliotangulia
Ukurasa 3 wa 6
Ukurasa unaofuatia