You need to enable JavaScript to run this app.
Nenda kwenye maudhui
Nenda kwenye orodha kuu
Nenda tovuti zaidi za DW
Vidio zetu
Sauti zetu
Maeneo
Tanzania
Kenya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Afrika
Ulaya
Mada
Haki za binadamu
Mazingira
Afya
Teknolojia
Kategoria
Matukio ya Kisiasa
Masuala ya Jamii
Michezo
Yanayoangaziwa
Mzozo wa Kongo Mashariki
Mzozo wa Israel na Hamas
Bundesliga
Sauti zetu
Vidio zetu
Matangazo
Picha: DW
Vidio zetu
Tazama vidio zetu hapa
Ruka sehemu inayofuata Maudhui yote kwenye mada hii
Maudhui yote kwenye mada hii
Msichana Jasiri: Loistracy Andrew na athari za ukeketaji
Msichana Loistracy atumia sauti yake kukabiliana na athari za ukeketaji. Matumaini yake ni kuwa sauti ya mabadiliko
Ushawishi wa muziki katika jamii
Muziki una ushawishi mkubwa mno katika jamii - ni sauti iliyo na nguvu isiyoonekana na inayogusa mioyo ya watu, kubadilisha fikra na kuleta mabadiliko ya kijamii kwa njia ya kipekee. Muziki huathiri karibu kila nyanja ya maisha ya binadamu na kuunganisha watu bila kujali lugha, dini au asili. Je, unapenda kusikiliza muziki wa aina gani? Muziki umekuathiri kwa namna gani?
Msichana anayepiga vyombo vya muziki
Caren ni msichana wa miaka 10, lakini sauti na midundo yake ni mikubwa kuliko umri wake. Anapiga vyombo vya muziki na pia huimba kwa ustadi mkubwa. Ameshawahi kutumbuiza katika matamasha makubwa, na hata kutunukiwa cheti cha muziki. Bado ana ndoto ya kuliiwakilisha taifa lake katika majukwaa makubwa ya kimataifa kupitia muziki.
Macron akiri Ufaransa iliendesha vita dhidi ya Cameroon
Sehemu kubwa ya Caneroon ilitawaliwa na Ufaransa baada ya kushindwa kwa mtawala wake wa zamani wa kikoloni, Ujerumani
Msichana anayeongoza watalii majini
Kutoka kwenye pwani ya Tanzania hadi kwenye kina cha bahari, amegeuza hofu kuwa ujasiri na ndoto kuwa kazi.
Msichana anayetumia taka za plastiki kubuni bidhaa
Sarafina ni msichana mbunifu anayetumia taka za plastiki kubuni bidhaa.
Wanawake 5 wa Kiafrika wanaobadilisha dunia
Katika kuadhimisha Siku ya Wanawake wa Kiafrika, tunatambua mchango wa wanawake ambao wanavuka mipaka ya jadi na kuleta mabadiliko makubwa katika jamii zao - kutoka kwenye uongozi wa sekta za mabilioni hadi mapambano dhidi ya sumu na ukosefu wa haki. Katika Siku ya Wanawake wa Afrika, tunamulika simulizi zao.
Kipi bora kati ya kazi za mikono na taaluma ya masomo?
Mjadala kuhusu kipi bora kati ya kazi za mikono na taaluma ya masomo ni mpana na wenye hoja nzito kwa kila upande. Kwa wanaounga mkono kazi za mikono wanasema ujuzi wa mikono hutoa ajira haraka na kwa wingi huku mafundi wakitatua matatizo halisi ya kila siku – maji, umeme, ujenzi na kadhalika. Je, ukipewa nafasi ya kuchagua kati ya kazi za mikono na taaluma ya masomo, utachagua ipi?
UN: Suluhu ya mzozo wa Gaza ni mataifa mawili
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema kwenye Mkutano wa Ngazi ya Juu wa Kimataifa kuhusu Usuluhishi wa Amani wa Suala la Palestina na Utekelezaji wa Suluhu ya Nchi Mbili za Israel na Palestina kwamba "Suluhu pekee ya kweli ya haki na endelevu katika mzozo wa Gaza ni mataifa mawili, Israel na Palestina.
Buminganyikani, msichana mdogo anayewasaidia wenzake
Buminganyikani ni msichana wa kidato cha sita ambaye amekuwa akitumia muda wake katika kutembelea vituo vya watoto.
Muongozo wa mavazi kwenye vyuo vikuu
Mavazi ya staha chuoni ni suala linalozua mjadala mpana, ingawa lina umuhimu katika muktadha wa kijamii, kitaaluma na hata kimaadili. Mwanafunzi hasa wa chuo kikuu anastahili kuvaa mavazi ya staha na heshima chuoni. Je, kuna umuhimu wa kudhibiti aina ya mavazi katika vyuo vikuu vya umma?
Msichana Jasiri: Faith na uthubutu wa kuongea na umati
Kutana na Faith Fransis binti wa miaka 8 alojipatia umaarufu mitandaoni kwa kujieleza mbele ya umati.
Mchana daktari, usiku mwanamuziki...
Nchini Rwanda, jina la Dkt. Thomas Muyombo linavuma hata nje ya kuta za hospitali. Anajulikana na wengi kwa jina lake la kisanii Tom Close, na ni mwanamuziki maarufu! Mchana ni daktari, usiku ni mwanamuziki. Hii imekaaje? Tizama video. Juni 27, 2025 #Kurunzi #DwKiswahili
Binti aliyejitosa kutunza mazingira Tanzania
Msichana jasiri wiki hii inamulika juhudi zinazofanywa na binti Ilakiza katika uhamasishaji wa kutunza mazingira nchini Tanzania. Anawaelemisha vijana wenzake kuhusu athari za mabadiliko ya tabianchi, uchafuzi wa mazingira, na umuhimu wa kuhifadhi vyanzo vya maji na misitu. #msichanajasiri #vijana #mazingira #tabianchi #tanzania
Uganda:Mjue kinda wa muziki wa "rap" nchini Uganda
Uganda:Mjue kinda wa muziki wa "rap" nchini Uganda
Uthubutu wa kuanzisha jukwaa la vijana mtandaoni
Doricas ni msichana wa miaka 20 ambaye ameanzisha jukwaa la kuwakutanisha vijana kuanzia miaka 15–25.
Msichana Jasiri: Mwanzilishi wa programu ya afya ya Akili
Adila Nassoro wa Tanzania aliamua kuanzisha programu ya kipekee dhidi ya unyanyapaa wa afya ya akili
Msichana Jasiri: Ijumaa Kuu
Wasichana wazungumzia umuhimu wa siku ya Ijumaa Kuu
Tiba asilia za mifupa ni salama kwa kiasi gani?
Wapo watu wengi wanaoamini katika tiba asilia ya kuunganisha mifupa na viungo vingine vya mwili vilivyoteguka au kuvunjika pasi ya kuenda hospitalini. Swali ni je, tiba hizo ni salama kwa kiwango gani? Tumekuandalia mtizamo wa pande zote mbili ikiwemo kauli ya mhazigi yaani daktari bingwa wa mifupa hospitalini.
Kutana na msichana anayepiga vita rushwa ya ngono
Joanitha ni mwanafunzi anayesomea masuala ya ustawi wa jamii. Anapinga masuala ya rushwa ya ngono kwa wasichana.
Ufahamu ugonjwa wa findofindo kwa watoto
Ni ugonjwa wa tezi za kinywa ambao huwaathiri watu wote wakiwemo watoto pia. Tezi hizi husaidia kupambana na vimelea vinavyoingia kwenye mwili kupitia kinywa.
Taaluma yako inaweza kulinda afya ya jamii?
Faraja kama lilivyo jina lake, anayo ari na dhamira ya kweli ya kuleta mabadiliko katika jamii kupitia elimu ya afya. Akiwa mwanafunzi wa udaktari, ametumia maarifa anayoyapata chuoni kuelimisha jamii kuhusu magonjwa yasiyo ya kuambukiza ambayo yanachangia idadi kubwa ya vifo vya watu duniani.
Christine Miundi, mwanamke aliyeishinda Fistula Kenya
Kutana na Christine Muindi anayesimulia jinsi Fistula ilivyobadilisha maisha yake.
Wasichana na matumizi ya Akili Bandia
Ni wasichana watatu walioamua kuwaelimisha wengine namna ya matumizi ya akili bandia katika kutafuta suluhu za changamot
Mafuriko Kinshasa
Watu 30 wamefariki dunia Kinshasa kufuatia mafuriko yaliyoukumba mji huo mwishoni mwa wiki. Serikali inawalaumu waliojenga makaazi karibu na mito na imetishia kuwafurusha. Mto Ndjili ambao unapitia sehemu moja ya mji huo mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, ulifurika na kuvunja kingo zake. Gavana wa Kinshasa Daniel Bumba Lubaki anasema miundombinu ya maji imeathirika.
Msichana Jasiri: Shadya Kitenge, mbunge wa viti maalum UDSM
Shadya kitenge ni mbunge wa viti maalum katika chuo kikuu cha Dar es Salaam. Shadya amekuwa katika mstari wa mbele kuwahamasisha wasichana wenzake kujiamini na kuthubutu kuwania nafasi za uongozi. Amekuwa alama na ushawishi kwa wasichana wengine kutamani kuwania nafasi za uongozi mbali na chuo.
Wasichana wajiandaa na sikukuu ya Eid
Zimesalia siku chache waumini wa dini ya kiislamu kukamilisha ibada muhimu ya funga, inayofuatiwa na shamrashamra za sikukuu ya Eid. Wasichana wamejipanga kusherehekea siku hiyo kwa namna gani?
Kurunzi Wanawake: Daktari bingwa wa upasuaji pwani ya Kenya
Kurunzi Wanawake leo inamuangazia daktari Maryam Badawy ambaye ameingia kwenye historia katika tasnia ya tiba kwa kuwa mwanamke wa kwanza katika eneo la pwani ya Kenya kuwa daktari bingwa wa upasuaji wa kurekebisha maumbile. Daktari Maryam amekuwa alama ya matumaini kwa wanawake wanaopambana na saratani ya matiti.
Mfahamu Nyanya Rukia mchekeshaji kutoka Kenya
Safari yake ya sanaa haikuwa rahisi, alianza na kile alichonacho kwenye jamii yake ambayo ilimpokea na kumuunga mkono na sasa ni mtengenezaji maudhui ya mtandaoni, kando yake ni Ahmed Hassan mchekeshaji wa aina yake kutoka uraibu wa mihadarati hadi kinara kwenye jamii ya watu wa Mombasa.
Rozy: Kutoka mwanajeshi idara ya vilipuzi hadi makanika
Kama wasichana wengine wenye ndoto ya kuwa watu wa kutegemewa kwenye mataifa yao, alitamani kuwa mwanajeshi kwenye idara ya vilipuzi lakini mambo hayakuwa upande wake na kujikuta kwenye taaluma ya magari kama makanika. Hapo anatamani pia kufungua karakana itakayowaajiri wasichana na wanawake tu.
Rebecca: Msichana aliyegundua programu ya kuchagua vyuo
Rebecca ni msichana aliyebuni programu tumizi kwa ajili ya kuwasidia watu kuchagua vyuo kutokana na ufaulu. Programu hii inalenga kuwasaidia wanafunzi na watu wanaotaka kujiunga na vyuo vikuu kutafuta fursa kulingana na matokeo yao. #msichanajasiri
Haki za wanawake hatarini miaka 30 tangu azimio la Beijing
Vitisho hivi ni pamoja na ubaguzi, ulinzi dhaifu wa kisheria, na upungufu wa ufadhili kwa taasisi za kulinda wanawake.
Vijana wanakumbana na yapi wakati wa Kwaresma na Ramadhan?
Wakati waumini wa Kiislamu wakiwa kwenye mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan na baadhi ya madhehebu ya Kikristu yakitarajiwa kuanza Kwaresma kuanzia siku ya Jumatano, bado kuna fikra tofauti kuhusu kutimizwa kwa ibada hizi. Je, wewe una mtizamo gani katikati ya mabadiliko kuanzia ya mazingira na sayansi na teknolojia? Tizama video hii, kisha utupe maoni yako. #kurunzi
Kurunzi Afya - Siku ya Kusikia Duniani
Ulimwengu leo unaadhimisha siku ya kusikia duniani. Utafiti uliofanywa na shirika la afya duniani WHO umeonyesha kuwa zaidi ya watu milioni 400 wanahitaji msaada wa kuwezeshwa kusikia. Wataalam wa afya wametahadharisha juu ya kusikiliza muziki kwa sauti kubwa na kwamba tatizo la watu kutosikia linaendelea kukua kwa kiwango cha kutia wasiwasi.
Msichana Jasiri - Sarafina Simioni - Mwanaharakati wa Jinsia
Katika jamii inayotawaliwa kwa sehemu kubwa na mfumo dume, inahitaji ujasiri wa kipekee kusimama na kutetea haki za wanawake na wasichana. Sarafina Simioni, binti mdogo lakini mwenye sauti kubwa, ni miongoni mwa mashujaa wa zama hizi. Ni mwanaharakati shupavu wa masuala ya jinsia nchini Tanzania, anayejituma kuelimisha na kuhamasisha jamii kuhusu haki za wanawake na wasichana.
Mfahamu Lina msichana muelimishaji juu ya hedhi salama
Elimu yake inawasaidia kujenga ujasiri, kuwa na afya bora, na kuwa na uelewa wa haki zao za kimwili.
Ujerumani chini ya NATO yaanza doria Bahari ya Baltic
Ujerumani inashiriki katika oparesheni mpya ya NATO inayolenga kuongeza ufuatiliaji na kuchunguza uwepo wa hujuma katika Bahari ya Baltiki. Hatua hii ni baada ya kuongezeka kwa visa vya uharibifu wa miundombinu chini ya bahari katika eneo hilo.
Hospitali mjini Goma zazidiwa na majeruhi wa vita
Wakati mapigano yakisimamishwa kati ya jeshi na kundi la waasi la M23 ili kupisha misaada na huduma za kiutu kwa raia nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, hospitali zimehelemewa na idadi kubwa ya majeruhi wa vita, huku kunashuhudiwa uhaba wa dawa na wahudumu wa afya.
Makanika mwanamke aliyegeuka kivutio Busia, Kenya
Kinyume na matarajio ya wengi, Florence huchukua spana kwa ustadi na kushughulikia injini za magari kwa ujasiri usio wa kawaida. Licha ya mashaka kutoka kwa baadhi ya watu waliodhani kazi hii ni ya wanaume pekee, ameweza kuthibitisha kuwa ujuzi na bidii havibagui jinsia.
Je, vijana wameandaliwa vyema katika uwekezaji?
Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, zaidi ya asilimia 60 ya watu katika eneo la Afrika Mashariki ni vijana walio na umri wa chini ya miaka 30. Wachumi wanaitaja kuwa hiyo ni fursa kubwa kwa maendeleo. Je, vijana wamejiandaa na kuandaliwa vyema katika seka ya uwekezaji?
Haluwa kitinda mlo maarufu pwani ya Afrika Mashariki
Wenyeji wa pwani ya Afrika Mashariki hufurahia kitinda mlo hiki hasa majira ya jioni, kinaandaliwa kwa namna tofauti lakini walaji wanasema wanavutiwa zaidi na ile iliochanganywa kwa ustadi mkubwa na viungo vya asili.
Msichana Jasiri: Fursa katika dansi la mtaani
Dansi ni moja ya fursa kwa vijana wa dunia ya sasa, kundi la washichna wadogo kutoka jiji kuu la kibiashara Tanzania, Dar es salaam, wameanzisha kundi lao kwa ajili ya kunoa talanta na kusaka fursa hizo kupitia majukwa ya kidigitali.
Jackline Malavanu: Mtunzi wa Mashairi
Jackline Malavanu ni mtunzi mahiri wa mashairi anayejulikana kwa ustadi wake wa kipekee wa kutumia maneno.
Historia ya wanawake Namibia enzi za ukoloni inavyosimuliwa
Wanawake wa Namibia walishuhudia na kupitia kwanza mauaji ya halaiki ya enzi ya ukoloni wa Ujerumani. Na hii leo, wanawake ndiyo wako mstari wa mbele kukuza ufahamu wa kilichotokea na kuganga yajayo.
Wanawake wa Namibia na uasi dhidi ya ukoloni
Uvamizi wa kikoloni wa Ujerumani nchini Namibia dhidi ya jamii za Nama na Herero ulimaanisha vita vya jamii nzima, siyo vya askari pekee. Manusura walipitia madhila ya kutisha, lakini wanawake walistahamili na kupambana kuihami jamii yao.
Tamaduni zilivyochochea jamii kupambana na ukoloni
Katika mwendelezo wa Makala za kivuli cha ukoloni wa Ujerumani, tunatizama jinsi tamaduni zilizisaidia jamii kuchukua msimamo dhidi ya utawala wa kikoloni. Mwishoni mwa miaka ya 50 wanawake waliilazimisha serikali ya kikoloni nchini Cameroon kuachia ngazi. Nchini Cameroon, kuna utamaduni wa karne nyingi unaoitwa Anlu.
Uasi uliofanywa na jamii ya Dahomey huko Cameroon
Mwaka 1893 wanaume na wanawake wa Dahomey walifanya uasi mkubwa dhidi ya unanyanyasaji wa maafisa wa kikoloni wa Ujerumani nchini Cameroon, katika mojawapo ya vuguvugu kubwa ambalo Ujerumani haikuwa imejiandaa. Tizama simulizi hiyo.
Li'ti Kidanka alifahamika zaidi kama Malkia wa Nyuki
Wakoloni wa Kijerumani walipoingia Afrika Mashariki, walikutana na nguvu ambayo hakuna aliyekuwa ameitarajia ya Li'ti Kidanka. Li’ti Kidanka alikuwa kiongozi wa kiroho kutoka jamii ya kabila la WaNyaturu mkoani Singida, kanda ya Kaskazini-Kati mwa Tanzania.
Nduna Mkomanile, shujaa wa kike Tanzania enzi ya ukoloni
Katika mfululizo wa Makala za video zilizoandaliwa na DW, tunatizama jinsi gani ukoloni wa Ujerumani Afrika ulivyokabiliwa na upinzani mkali. Nduna Mkomanile ambaye alijitahidi kuziunganisha jamii za Tanzania dhidi ya ukoloni wa Wajerumani wakati wa vita vya Maji Maji mwanzoni mwa karne ya 20. Sasa anatambulika kama mmoja wa mashujaa wa kike muhimu zaidi wa uhuru wa Tanzania.
Mfahamu nyota chipukizi katika filamu Tanzania
Najma Juma ni mwigizaji anayechipuka kwa kasi katika tasnia ya filamu. Kwa kipaji cha kipekee na juhudi zisizo na kikomo, amekuwa akivutia macho ya watazamaji na wataalamu wa filamu. Ingawa ni mpya kwenye tasnia, licha ya juhudi zake amekuwa akikumbana na changamoto kubwa ya kukatishwa tamaa katika mitandao ya kijamii lakini kwake anaitumia kama chachu ya kufikia malengo yake.
Ukurasa uliotangulia
Ukurasa 1 wa 6
Ukurasa unaofuatia