VATIKAN CITY : Papa awaambia Waafrika washikilie msimamo wa kutozini
11 Juni 2005Matangazo
Papa Benedict 13 amewaambia maaskofu wa kusini mwa Afrika hapo jana kwamba mafundisho ya Kanisa Katoliki ya kutozini na kuwa mwaminifu kwenye ndoa ni njia pekee za uhakika za kuzuwiya kuenea kwa UKIMWI.
Mafundisho hayo yanaendelea kubakia sambamba na msimamo uliokuwa ukitetewa kwa muda mrefu na mtangulizi wake Papa John Paul wa Pili ambaye amelaani matumizi ya kondomu na kutetea kutozini na kuwa mwaminifu kama njia pekee za kuzuwiya gonjwa hilo thakili.
Papa huyo mzaliwa wa Ujerumani pia amewataka maaskofu hao kuweka nadhari maalum katika mafunzo ya makasisi kwa kusema kwamba dunia iliojaa vishawishi inahitaji makasisi ambao wamejizatiti kwa kazi zao.