Vatican,Baba Mtakatifu arejeshwa tena hospitalini baada ya kukumbwa na homa ya mafua makali.
24 Februari 2005Matangazo
Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani,Papa John Paul wa pili,amerejeshwa tena hospitalini baada ya kurejewa na homa ya mafua makali.Taarifa kutoka makao makuu ya Papa mjini Vatican,imeeleza kuwa Baba mtakatifu anahitaji matibabu maalum.
Madaktari wake wamependekeza kuwa arejeshwe katika hospitali ya Gemelli mjini Rome.
Kiongozi huyo wa Wakatoliki duniani ambaye kwa sasa anaumri wa miaka 84,anasumbuliwa na maradhi kadhaa yakiwemo yale ya kukakamaa viungo vya mwili.
Mapema mwezi huu alilazwa kwa muda wa siku 10 hospitalini,baada ya kukumbwa na matatizo makubwa ya kupumua.