VATICAN-Wosia wa Baba Mtakatifu watolewa.
7 Aprili 2005Matangazo
Wosia wa mwisho ulioandikwa na Baba Mtakatifu Yohanne Paulo wa pili umetolewa na unaonesha kuwa katika mwaka 2000 alikereka kutokana na suala la iwapo ajiuzulu,baada ya kuliongoza Kanisa Katoliki katika millenium mpya.Katika wosia huo wa maandishi ulioandikwa zaidi ya miongo miwili iliyopita,Baba Mtakatifu pia ameonesha kuwa siku za mwanzo za kutumikia kama Baba Mtakatifu,alikuwa anafikiria akifa azikwe kwao Poland.
Makao makuu ya Papa mjini Vatican yamesema kuwa Baba Mtakatifu baadae akaamua kuacha kila jambo liamuliwa na Makadinali wa kanisa Katoliki.