VATICAN. Viongozi wa Vatican warudishwa tena kwenye nyadhifa zao.
21 Aprili 2005Matangazo
Makao makuu ya kanisa katoliki, Vatican, yametangaza kwamba papa Benedict wa 16 amewarudisha maafisa wa ngazi ya juu wa Vatican katika nyadhifa zao. Kadinali Angelo Sodano wa Itali, anayechukua nafasi ya pili baada ya papa, ni miongoni mwa waliorudishwa madarakani.
Watu wasiopungua elfu 50 na viongozi wa mataifa mbalimbali wanatarajiwa kuhudhuria misa ya kumtawaza papa Benedict wa 16 mjini Rome Jumapili ijayo, ikiwa yanakaribia majuma mawili tangu umati ulipokusanyika kumuaga marehemu Yohana Paulo wa pili.