JamiiVatican
Vatican: Papa Francis anaendelea vizuri
5 Machi 2025Matangazo
Papa Francis lakini ameshindwa kuongoza ibada muhimu ya Jumatano ya Majivu, inayofungua kipindi cha siku 40 za mfungo wa Kwaresma.
Kwa kawaida Papa Francis mwenye umri wa miaka 88 huongoza ibada hiyo, lakini kwa leo misa hiyo itaongozwa na Kadinali wa Italia Angelo de Donatis, na kutanguliwa na maandamano kwenye kilima cha Aventine huko Roma.
Kulingana na imani ya dini ya Kikristo, mfungo wa Kwaresma hufanyika siku 40 kabla ya sherehe ya Pasaka ikikumbushia siku alizozitumia Yesu Kristo kufunga akiwa jangwani.