VATICAN. Papa Benedict wa 16 aongoza misa yake ya kwanza.
21 Aprili 2005Matangazo
Papa Benedict wa 16 aliongoza misa ya kwanza tangu kuchaguliwa kwake Jumanne iliyopita. Kiongozi huyo alitumia misa hiyo kuwatolea wito makadinali wake kumuunga mkono na kumuombea. Alitoa heshima zake kwa marehemu Yohana Paulo wa pili, akisema alikuwa kiongozi shujaa.
Papa Benedict wa 16 alisema anataka kuwaunganisha wakristo wote na kufanya mazungumzo ya kuaminika na waumini wa dini nyengine. Alithibitisha pia kwamba atafanya ziara yake ya kwanza ya kigeni nchini mwake Ujerumani. Anatarajiwa kuhudhuria sherehe za siku ya vijana zitakazofanyika mwezi Agosti katika mji wa Cologne, hapa Ujerumani.