VATICAN: Hatimae baba mtakatifu azikwa katika mazishi ya kihistoria.
8 Aprili 2005Matangazo
Hatimae mwili wa baba mtakatifu ulizikwa mchana wa leo katika chumba cha siri kilicho chini ya kanisa la mtakatifu Petro mjini Roma.
Baada ya mazishi mlio mmoja wa kengele ulisikika kutoa ishara ya kuwa mazishi yamekamilika.
Mamilioni ya watu walihudhuria shughuli za mazishi ya baba mtakatifu ambako zaidi ya viongozi 200 wa tabaka mbalimbali walijumuika na waombolezaji wengine katika mazishi hayo ya kihistoria.
Shughuli ya mazishi iliongozwa na kadinali wa kijerumani Joseph Ratzinger ambae pia ni mkuu wa chuo cha makasisi.
Rais Horst Köhler aliwakilisha Shirikisho la jamuhuari ya Ujerumani akiwa ameandamana na kansela Gerhard Schröeder.