ImaniVatican
Vatican: Hali ya Papa Francis inafuatiliwa kwa uangalifu
1 Machi 2025Matangazo
Tarifa hiyo imeendelea kueleza kuwa hapo jana Papa Francis mwenye umri wa miaka 88, alitapika mara kadhaa huku njia za hewa zikikabiliwa na matatizo yaliyopelekea kuunganishwa na mashine za kumsaidia kupumua. Hayo ni baada ya hali yake kuripotiwa kuwa mbaya Ijumaa alasiri kutokana na shinikizo la kupumua.
Soma pia: Mamia ya watu wahudhuria misa maalum kumuombea Papa
Vatican imeendelea kuwa hali ya Papa Francis ambaye amelazwa katika hospitali ya Gemelli mjini Rome kwa zaidi ya wiki mbili, sasa inafuatiliwa kwa uangalifu mkubwa.