JamiiVatican
Vatican: Hali ya kiafya ya Papa Francis yaimarika
20 Machi 2025Matangazo
Taarifa hiyo iliyotolewa Jumatano usiku imeendelea kuwa kiongozi huyo wa kidini mwenye umri wa miaka 88 na ambaye amelazwa hospitalini mjini Rome kwa zaidi ya mwezi mmoja, sasa hana homa na wala haitaji tena kutumia vifaa vya kumsaidia kupumua.
Soma pia:Papa Francis ataendelea kubakia hospitali kwa matibabu
Hata hivyo Vatican bado haijatoa muda ambao Papa Francis ataruhusiwa kutoka hospitalini, ikisema kuwa hali yake inaimarika taratibu, lakini ikasisitiza kuwa ataendelea na shughuli zake akiwa hospitalini. Waaumini kote duniani wameendeleza ibada za kumuombea Kiongozi huyo mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani.