VATICAN: Baba mtakatifu aombea amani Togo.
2 Mei 2005Matangazo
Baba mtakatifu Benedict wa 16 alongoza misa ya kwanza ya baraka kwa maelfu ya waumini waliohudhuria katika uwanja wa kanisa la mtakatifu Petro hapo jana.
Katika hotuba yake ya kuadhimisha siku ya wafanyakazi duniani, baba mtakatifu alitaka heshima na ubinadamu vidumishwe katika sehemu za kazi.
Baba mtakatifu pia alitoa hoja ya kutafutwa suluhisho la amani huko nchini Togo na mataifa yote yanayo kabiliwa na mizozo na umasikini.
Kwengineko baba mtakatifu Benedict wa 16 alihamia rasmi katika makao yake ya papa siku ya jumamosi.