VATICAN-Baba mtakatifu alishwa chakula kwa kupitishiwa mirija puani.
31 Machi 2005Matangazo
Makao Makuu ya Baba Mtakatifu mjini Vatican,yameeleza kuwa Baba Mtakatifu Yohanne Paulo wa pili kwa sasa analishwa chakula kwa kutumia mirija inayopitishwa puani.Madaktari wameeleza kuwa kushindwa kwake kumeza chakula kwa njia ya kawaida,huenda ni matokeo ya maradhi yanayomkabili ya kukakamaa viungo.
Mwezi uliopita wa Februari,Baba Mtakatifu alifanyiwa upasuaji katika koo lake kumsaidia kupumua vizuri.
Kabla ya kuwekewa mirija ya kupitishia chakula puani,Baba Mtakatifu jana alionekana katika dirisha lake akiwasalimia watu waliofika katika viwanja vya kanisa la Mtakatifu Petro kumtakia afya njema.Hata hivyo alishindwa kuzungumza vizuri katika muda wa dakika nne alijitokeza dirishani kwake.