Vance apigia debe sera rafiki kwa AI
11 Februari 2025Matangazo
Akizungumza kwenye mkutano wa kimataifa kuhusu Akili Mnemba unaofanyika mjini Paris, Vance ameonya kwamba udhibiti mkali wa teknolojia hiyo utapunguza ubunifu na matarajio ya kufikiwa enzi mpya ya mapinduzi ya viwanda. zaidi anasema "Tunaamini udhibiti uliopindukia wa AI utaiua sekta hiyo ya kimapinduzi wakati ndiyo inaanza kukua, na tutafanya kila tunaloweza kupigia debe sera za kuikuza AI, na ningependa kusikia zaidi hilo kwenye majadiliano ya mkutano huu" Mkutano huo wa siku tatu ulioitishwa na Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa, unatarajiwa kutoa azimio la kimataifa la usimamizi na udhibiti wa teknolojia ya AI inayokua kwa kasi kwenye mataifa mengi yaliyoendelea.