JD Vance aishutumu Denmark kwa kushindwa kuilinda Greenland
29 Machi 2025Matangazo
Makamu wa Rais wa Marekani JD Vance ameishutumu Denmark kwa kushindwa kuilinda Greenland kiusalama, wakati wa ziara yake katika kisiwa hicho cha Arctic ambacho kinakodolewa macho na Rais Donald Trump.
Vance na mkewe, Usha, walikuwa ni sehemu ya ujumbe wa Ikulu ya White House, waliotembelea kambi ya kijeshi ya Marekani huko Greenland, eneo linalojitawala ambalo ni sehemu ya Denmark.Kiongozi wa Greenland akutana na Mfalme wa Denmark
Ziara ya Makamau wa Rais Vance inatizamwa na Copenhagen na Greenland kama uchokozi, kufuatia matamshi ya Trump ya kutaka kukimiliki kisiwa hicho.
Trump anadai kuwa Marekani inakihitaji kisiwa hicho kikubwa cha Arctic kwa usalama wa kitaifa na kimataifa na amekataa kuondoa wazo la matumizi ya nguvu kukidhibiti.