Uwezekano upo wa Urusi na Ukraine kufikia amani
15 Aprili 2025Steve Witkoff, ambaye ni mjumbe maalum wa Rais wa Marekani Donald Trump amesema Rais wa Urusi Vladimir Putin yuko tayari kufikia makubaliano ya "amani ya kudumu" na Ukraine, baada ya mazungumzo yenye lengo la kumaliza vita vilivyodumu kwa zaidi ya miaka mitatu kati ya Urusi na Ukraine.
Mjumbe huyo maalum wa Marekani alikutana na Rais Putin huko Saint Petersburg ukiwa ni mkutano wao wa tatu wa tangu Rais Donald Trump arejee ikulu ya Marekani mnamo mwezi Januari.
Wakati huo huo Urusi imesema vikosi vya Ukraine vimefanya mashambulizi ya ndege zisizo na rubani katika eneo la Kursk lililo mpakani kati ya Urusi na Ukraine. Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 85 ameuawa. Watu tisa wamejeruhiwa na vilevile shambulio hilo limesababisha moto kwenye majengo kadhaa.