JamiiUingereza
Uwanja wa ndege wa Heathrow wafunguliwa tena
22 Machi 2025Matangazo
Safari za ndege katika uwanja huo wa Heathrow zimeanza taratibu baada ya kukatizwa kwa saa 18 na hivyo kuathiri wasafiri zaidi ya 200,000.
Soma pia: Moto wasababisha uwanja wa Heathrow kufungwa
Kwa mujibu wa mashirika yanayofuatilia safari za ndege, takriban abiria 230,000 kwa siku na milioni 83 kwa mwaka, hutumia uwanja wa Heathrow, na hivyo kuufanya kuwa miongoni mwa viwanja vyenye shughuli nyingi zaidi duniani.