Mtandaoni, ofa inaonekana kuwa ya kweli sana: Unapata figo mpya ndani ya wiki chache tu. Ni mwanzo wa maisha mapya bila mahangaiko ya ‘dialysis’. Nyuma ya yote haya, kuna mtandao wa wafanyabiashara wa viungo wanaosakwa kimataifa. Hii ni ripoti maalum ya uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa DW nchini Kenya kwa ushirikiano na Der Spiegel na ZDF.