Uturuki yaomba ushirikiano kupambana na wapiganaji wa PKK
26 Januari 2025Fidan ametoa wito huo Jumapili akiwa ziarani Baghdad. Ziara ya Waziri huyo wa mambo ya nje wa Uturuki huko Baghdad inafanyika baada ya taarifa kuwawalinzi wawili wa mpaka karibu na Uturiki waliuwawa Ijumaa katika shambulio ambalo Iraq imesema lilifanywa na PKK.
Soma zaidi: Uturuki imesema imesambaratisha maghala ya wanamgambo wa PKK pamoja na kuwaua baadhi yao
Hivi karibuni, Iraq imeongeza makali dhidi ya chama hicho. Mwaka uliopita, ilikiorodhesha kama kundi lililopigwa marufuku licha ya kuwa Ankara inaitaka Baghdad ifanye juhudi zaidi katika kupambana nacho.
Wapiganaji wa Chama cha wafanyakazi cha Wakurdi cha PKK kinachopambana dhidi ya Uturuki kwa miongo kadhaa sasa, wapo katika eneo linalojitawala la Kurdistan la Iraq ambalo pia lina ngome za kijeshi za Uturuki.