Uturuki na Syria wasaini mkataba wa ushirikiano na ulinzi
14 Agosti 2025Matangazo
Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Ulinzi ya Uturuki iliyochapishwa kwenye tovuti yake, Mkataba huo unajumuisha mafunzo ya pamoja na ushauri, bila ya kutoa maelezo kamili.
Katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari uliofanyika Ankara, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Hakan Fidan, alitoa wito kwa wanamgambo wa Kikurdi wa YPG kuondoa uwepo wao kama tishio kwa Uturuki na eneo zima.
Huku haya yakijiri, Tume ya Umoja wa Mataifa kuhusu Syria imeitaka serikali ya mpito kuongeza juhudi zake za kuhakikisha uwajibikaji, ikisisitiza kuwa kiwango kikubwa cha ukatili kilichoshuhudiwa kinastahili hatua madhubuti zaidi.