Sheria na HakiAsia
Utawala Myanmar waongeza muda wa hali ya dharura
31 Januari 2025Matangazo
Baraza tawala la kijeshi linaloongozwa na mkuu wa jeshi, Min Aung Hlaing, kwa kauli moja liliidhinisha hatua hiyo, hii ikiwa ni kulingana na vyombo vya habari vya serikali hiyo.
Hii inamaanisha kwamba uchaguzi ulioahidiwa kwa muda mrefu hauwezi kufanyika kutokana na hali hiyo ya hatari na kulingana na serikali, uchaguzi sasa utafanyika mwanzoni mwa nusu ya pili ya mwaka.
Soma pia:Utawala wa kijeshi nchini Myanmar waongeza muda wa hali ya dharura kwa miezi sita zaidi
Nchi hiyo ilitumbukia kwenye mzozo wa umwagaji damu uliotokana na mapinduzi ya Februari 1, 2021 yaliyohitimisha miaka 10 ya demokrasia nchini humo na kukiondoa chama cha Aung San Suu Kyi cha National League for Democracy (NLD) kilichokuwa kimeshinda uchaguzi wa 2020.