SiasaNiger
Niger yawaachia mawaziri wa serikali iliyopinduliwa
2 Aprili 2025Matangazo
Miongoni mwa walioachiliwa huru ni waziri wa zamani wa mafuta, Mahamane Sani Issoufou, ambaye ni mtoto wa rais wa zamani, Mahamadou Issoufou aliyetawala baina ya mwaka 2011 na 2021, waziri wa zamani wa ulinzi, Kalla Moutari, waziri wa zamani wa fedha, Ahmad Jidoud, na waziri wa zamani wa nishati, Ibrahim Yacoub.
Yumo pia mwenyekiti wa chama kilichokuwa kinatawala, Foumakoye Gado, mwanadiplomasia mmoja, mwandishi mmoja wa habari, Ousmane Toudou, na wanajeshi kadhaa waliokuwa wamehukumiwa kwa jaribio la mapinduzi mwaka 2010.
Hata hivyo, rais aliyeondolewa madarakani na jeshi, Mohamed Bazoum, bado yupo kizuizini licha ya miito ya kimataifa kutaka aachiliwe.