JangaMyanmar
Tetemeko:Jeshi na waasi wasitisha mapigano kwa muda Myanmar
3 Aprili 2025Matangazo
Hatua hiyo imetangazwa Jumatano kufuatia tetemeko kubwa la ardhi lililosababisha vifo vya watu zaidi ya 3,000, na baada ya makundi yenye silaha yanayoupinga utawala wa kijeshi, kutangaza hapo awali kwamba yanasitisha mapigano ili kudhihirisha mshikamano na wananchi katika janga hilo.
Juhudi za uokoaji zinaendelea huko Myanmar ambako pia watu zaidi ya 4,500 wamejeruhiwa. Jana, siku tano baada ya tetemeko hilo, watu kadhaa waliokolewa wakiwa hai katika baadhi ya maeneo ikiwa ni pamoja na kwenye mji wa Mandalay. Umoja wa Mataifa umesema watu milioni 3 wamelazimika kuyahama makazi yao na wanahitaji msaada wa dharura.