Jamii ya Wasuba nchini Kenya ni mojawapo ya makabila ya asili yaliyo na historia ya kipekee na tamaduni tajiri, ingawa kwa sasa jamii hiyo inakabiliwa na changamoto ya kutambuliwa na kuhifadhi utambulisho wao wa kitamaduni. Kwenye Makala ya Utamaduni na Sanaa, Musa Naviye anaiangazia jamii ya Wasuba wanaojitambulisha pia kama Abasuba.