Utafiti: Usitishaji misaada kulemaza miradi ya afya duniani
16 Julai 2025Matangazo
Utafiti huo uliochapishwa katika jarida mashuhuri la afya la Lancet, unaonesha ufadhili wa miradi ya afya itapungua kutoka dola bilioni 80 mwaka 2021 hadi dola bilioni 39 mwaka huu. Kiwango hicho ni cha chini zaidi kuwahi kushuhudiwa katika kipindi cha miaka 15 iliyopita.
Pengo hilo la ufadhili linalotokana na uamuzi wa kupunguza misaada uliochukuliwa na mataifa makubwa ikiwemo Marekani,Uingereza, Ufaransa na Ujerumani utalazimisha kuchukuliwa hatua kali za kubana matumizi katika sekta ya afya duniani.
Kulingana na utafiti huo, mataifa masikini kama Somalia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Malawi yataathirika vibaya na kupungua kwa fedha za miradi ya afya inayotegemewa na mamilioni ya watu.